Faidika na Methali, Nahau na Vitendawili

 

FAIDIKA NA METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI ni kitabu kilichoandikwa kwa ajili ya wanafunzi wa Kenya. Hata hivyo, kinaweza kutumika katika nchi yoyote ya Jumuia ya Afrika Mashariki na penginepo Kiswahili kinapozungumzwa. Katika mkusanyo huu, wanafunzi wa Shule za Msingi pamoja na walimu wao wataweza kufaidika kwa kuwa na kitabu kimoja chenye fani hizi - methali, nahau na vitendawili - zote katika fumbato moja. Msomaji anapokimaliza vyema kitabu hiki atakuwa amejiongezea msamiati na idadi kubwa ya methali, nahau na vitendawili. Aidha, atakuwa mweledi wa lugha ya kisanii (fasihi) kwani ataweza kubaini na kueleza ujumbe uliyomo kwenye methali, nahau na vitendawili, na pia kuzitumia fani hizo katika miktadha mbalimbali.

 

You can purchase this book on Amazon or IngramSpark