Usalama Barabarani

 

Idadi ya watu wanaokufa kila mwaka nchini Kenya kutokana na ajali za barabarani ni kubwa mno, kiasi kwamba ni lazima kila mtu ahusishwe katika kulitafutia tatizo hili suluhisho. Kitabu hiki kinaangazia mambo fulani yanayohusu usalama barabarani kwa lugha nyepesi. Kinaeleza juu ya njia bora za kutumia barabara kwa watembeaji kwa miguu, abiria, waendeshaji baisikeli na madereva wa magari; kile kinachosababisha ajali za barabarani na jinsi ya kuepukana nazo; huduma ya kwanza na vilevile jinsi ya kutekeleza kanuni za sheria za barabarani. Maelezo haya ni yenye manufaa makubwa kwa wanafunzi na watu wazima vilevile.

 

You can purchase this book on Amazon or IngramSpark